KARIBU KATIKA ULIMWENGU WA EMMANUEL

KARIBU KATIKA ULIMWENGU WA EMMANUEL
every successful person has a painful story and every painful story has a successful ending

Monday, February 27, 2012

KAZI INATAKA KUZALIWA NDANI YA KISIWA CHA MARASHI.

Kwa kawaida kabla ya kufanya shooting au kitu chochote ni lazima ufanye kwanza utafiti wa kina kwa ajili ya Shughuli hio. Sasa kwa mara ya kwanza watu wanafanya utafiti katika msitu mkubwa sana hapa Zanzibar na baadhi ya watu bada hawaja ujua. sio Jozani bali ni sehemu nyengine kabisa.
Vijana wakiwa na njaa kali ya kazi hapa ndio njia kuu ya kuingia katika pori hili...... wakishauriana mawili matatu kidogo
Eeee! kwa unavyo onekana msitu wenyewe.
Kijana wangu akiwa makini na uandishi na kwahasira ya njaa yake amevaa nguo ya kuto mzuia kupanda au kushuka katika msitu huu.
Safari ikipamba moto watu haoooooo
Kama kawaida yangu hua katika matukio na mimi niwepo kwa kuhakikisha mambo yanakwenda sawa. The one nikiwa ndani ya location
Jamani wadau na wapenzi wote huwezi kuamini chini ya msitu huu tulikuta kuna bonge la Mto yaani huwezi kujua kama uko Zanzibar na ndani ya mto huo kuna samaki wanao julikana kama Gold fish wametoka wapi mimi na wewe tusiulizane. ila kwakweli una pendeza sana. Hebu cheki mwenyewe.
unaona majani yalivyo tulia juu ya maji yani hadi raha.
ikanilazimu niweke kumbukumbu katika mto huo.
upande wa mashariki tulikuta kumbe kuna watoto ambao hua wana kuja kuvua wale samaki na kwenda kuwauza... jamani kwa wazazi ina bidi muwe makini maana hii inatisha msitu mkubwa kama huu ambao hata mtu mzima hawezi kwenda pekeyake ila watoto wana kwenda mwisho wake ita kua ni balaa kwahio tukae na watoto kwa umakini sana.
Hapa ntukiwa tunaondoka eneo hilo Burushi na Hamadi ikabidi nawao waweke kumbukumbu. ila semu hii itafanyiwa mambo mpaka wadau mtashangaa.
kazi ikiendelea kwa huku tukipata vitu ambavyotuna vihitaki babisaaaaaaaaaa.
Kama ndoto kumbe kweli tulikutana na ngombe wawili weupeee tena wako pekeyao na hawajafungwa.
Hamadi akiwa ana wachezea kidogo maana yeye anajiita ni mtu wa porini na haogopi kitu.

Safari ikiwa inaendelea na hapa ni sehemu ambayo sote tuliipeda kwa jinsi ilivyo na mandhati yake.
                                                       Baada ya kuzunguka sana ikabidi turudi
Jani si mchezo watu wakipanda milima kama uonavyo. Mungu akipenda tunategemea kuangusha moja ya Film katika msitu huu hivi karibuni ila Tuna mtanguliza kwanza Mungu aweze kutuongoza katika kila tunacho kifanya mana ni wengi wanao taka kuanza ila haja anza na kunawengine wana anza ila hawafanikiwi kumaliza na wengine pia wanamaliza ila hawafanikiwi kufanya vizuri katika kazi yao. Sasa sisi tuna muomba Mungu alie umba mbingu na nchi na kila kilichomo aweze kutusaidia kwa kila kitu na tuanze na kmualiza pamoja na kufanya vizuri kwenye kazi hii amen.