KARIBU KATIKA ULIMWENGU WA EMMANUEL

KARIBU KATIKA ULIMWENGU WA EMMANUEL
every successful person has a painful story and every painful story has a successful ending

Monday, May 21, 2012

HALIKUNIKI NA MIMI TUMEAMUA KUFANYA KAZI PAMOJA



Nina mshukuru mwenyezi Mungu, muumba wa mbingu na nchi ambae kwa yeye ndio kila kionekanacho chini ya jua na juu ya jua ni yeye alie fanya viwepo na vionekane. Mara nyingi mawazo ya binaadamu yanawaza katika maendeleo na mafanikio na ndio maana hata katika kitabu kitakatifu kinasema kua baada ya Mungu kumuumba binaadamu alimwambia alime na kuipalilia nchi. Jambo hili ni somo kubwa sana katika maendeleo ya mwana damu maana Mungu hakutaka Adam akae tu ila alitaka Adam afanye kazi na ndio maana pia Mungu alisema kua asie fanya kazi basi na asile. Mimi Emmanuel Obeid ( Emmanuel the one ) au Hoffy kwa wengi wanavyo nijua. Nime farijika sana baada ya kukubaliana kufanya kazi na Mzee wangu Halikuniki. Mzee huyu alikua anaonewa sana katika kazi hii na kujikuta akizulumiwa sana katika kazi alizo kua akishilikishwa katika tasnia hii ya film hapa Tanzania. Halikuniki mwenyewe anasema “ mimi Halikuniki nafurahi sana baada ya kukutana na wewe maana afadhali ninapo pa kukimbilia, Hapanchini wasanii na wananchi wote wananijua mimi ni nani maana mimi hua siigizi mimi ninafanya, sasa hivi hakuna msanii wa comedy maana wote wana igiza lakini mimi hata nikiwa nakula halafu ukanipiga picha basi unauza kwa hivi nilivyo. Mimi nimesomea sanaa katika chuo cha bagamoyo zamani, nasasa hivi nikienda mimi nadhani ndo nitakua mwalimu. Kutokana na hivi nilivyo watu wamekua wananitumia sana katika film zao na kuota vitambi kupitia mimi halafu mimi na baki nahangaika, kwani kunawatu wana toka dar es salaam wanakuja hapa na kunishilikisha katika movie zao kisha wana nipa shilingi 20 elfu. Wakinidanganya ila ndo naona kusaidiana na wengine hwanipi kabisa! Nachezeswa katika matangazo mbalimbali ya gharama za kulipwa milioni kwa dakika au lakitano ila wananidanganya na kwasababu ndo uzee na kua niko peke yangu nakua sina lakufanya. Ila kwa sasahivi nashukuru kukupata japokua ni mdogo sawa na mwanangu ila kutokana na wewe naona ndotozangu na mafanikio nitaenda kuyapata kwani hakuna wa kuweza kunishilikisha kwa lolote mpaka aonanane nawewe maana wewe ndo bosi wangu na kufunga makubaliano baina yangu mimi na wewe naona sasa sinto sumbuliwa tena maana mimi sinto hangaika watu wakinifuata na waambia kua waonane na wewe”.
Mzee Halikuniki alizungumza mengi haya ni kwaufupitu. Mimi na halikuniki tumekubaliana kufanya kazi pamoja na kusaidiana na tayari tumesha fanya kazi ambayo kwa sasa ndo tuko tuna malizia kufanya shooting na tupo katika hatua za mwisho kabisa. Pia kuna film nyingi ambazo zimesha andaliwa na kusu bili foleni na katika film zote hizo Halikuniki ameapa vya kufa kua sasa hivi nilazima watu wamjue kua yeye ndio Halikuniki. Katika movie hii mpya Halikuniki amebadilika kabisa japokua movie hii ina mandhali ya kijijini ila ni movie kali ambayo inaonekana kubadilisha mfumo wa tasnia ya film Tanzania na  Halikuniki amecheza kama baba yangu, ni stori ilio simama iko speed mwanzo mwisho ni furaha tu na haibagui wa kuangalia. 
                                                                         Kijana nime tulia.



THI IS HOW AM LOOK LIKE.

 We still in work so be cause of this movie am spouse to look like the villager man. Now I am look like this. 
                                                                               In left side.
                                                                        Other   side.
                                                                    Can I still be like this?

1 comment: