KARIBU KATIKA ULIMWENGU WA EMMANUEL

KARIBU KATIKA ULIMWENGU WA EMMANUEL
every successful person has a painful story and every painful story has a successful ending

Thursday, December 29, 2011

Dugu zanzu na wapendwa wangu napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru ninyi nyote mlio nisaidia kwa njia moja au nyengine katika kunifanikisha mambo yngu kuwa hapa yalipo ndani ya mwaka huu.
Hii niripoti ndogo tu ya baadhi yamambo ambayo yalifanyika katika kipindi chote tokea  january mpaka desmba.

1.       KIJAMII
Katika kipindi hiki mimi na kundi langu tuli tembelea sehemu mbalimbali za jamii ilio tuzunguka kwa kutembea na kutoa burudani kama vile vijijini, mijini na hata kwenye makanisa.

tukiwa katika kanisa la kwahani

baadhi ya matamasha

2.       KUHUSU KUNDI LANGU LA SANAA.
Napenda kuwashukuru wanachama wangu wa Extra genius arts group kwa mshikamano na umoja tulio uonesha katika mwaka huu jampo kulikua na changamoto za hapa na pale ila tumeendelea na mpaka sasa tuko sawa na niimani fangu kua mwaka huu tunao uanza utakua ni mwaka wa mafanikio makubwa kwa kundi na kwakila mwanachama tukianzia kimaisha, mana hakuna tunaemtegemea Zaidi ya Mungu alie umba mbigu na nchi.
Ndani ya mwaka huu tulipata mateso makubwa wakati wa kushoot fim maana mara nyengine ilitulazim kutembea kwa miguu mbali wa maili 8 kwa mguu huku tukuiwa tumebeba vifaavya shooting kweli ilikua ngumu ila tuliweza, tulikataliwa baadhi ya nyumba ambazo tulitaka kufanya shooting watu walitucheka, wenyemagari na pesa wengine walituahidi ila inafika sikuyasiku hamnakitu. Kwakweli mambu ya mwanzo wa mwaka 2011 yalikua na nguvu ila yalitupitisha katika wakati mgumu sana na kutokana na wakati huo ndio mana sasa tuko tuna enda katika wakati mzuri. Kikubwa kilicho tusaidia ni vikao na makubaliano.

vikao vikiendelea kama unavyo muona msanii mkongwa Halikuniki akitoa busarazake (wapili kutoka kusoto)

wakati tupo tuna tengeneza un biliverble hapo ilikua sine ya Myamba.namimi niki hakikisha watu wanafaya kazi kwa utuo.

manjonjo yalivyokua ndani ya movi hilo


MOVIE ZILIZO CHEZWA MWAKA 2011.
Katika kipingi cha mwaka 2011 tuliamua na kupendekeza kua tucheze movie mbili ambazo tuna mshukuru m\Mungu numefanikiwa kwa asilimia 98% ya kwanza ambayo tuliianza trahe 01/06/2011 ilio itwa UNBILIVERBLE tuliifanikisha jampo ndio ilio tutesa sana na yapili ina tegemewa kumalizwa tarehe 01/01/2012 jina liko kapuni na hii tumeifanya hivo makusudi ili mwaka utumalizie kazini na mwaka mwengine uingie tukiwa kazini kwa kutabiri kua mwaka huu unao anza ni kazi kwenda mbele hakuna kulala wala kupoteza muda.

3.       MAFANIKIO.
Tuna mshukuru Mugu kua mwaka huu umekua mwaka wa mafanikio makubwa katika kundi langu na hata mimi mwenyewe maana, katika mwaka 2011 tumeweza kucheza film na baadhi ya wasanii ambao walikuja kwaajili ya kusaidiana na kulisukuma hili kurudumu la tasnia ya film. Tmejulikana ndani na nje, wasanii kongezeka, nimezeza kushilikiana vizuri na wasanii wahapahapa Zanzibar hasa wakongwe wa sanaa. Tumetumia fifaa vya uhakika katika kushoot fim tofauti na zamani. Kipato kimekua kwa asuilimia nyingi ukilinganisha na mwaka 2009 na 2010.

gari ambalo hutusaidi wakati wa kazi


4.       WATU WALIOKUJA KUNITEMBELEA.
Nilipata wageni wengi sana ndani ya mwaka 2011 ambao wengine wanatoka ndani na wengine nje ya nchi kwajili ya kunitia moyo na kuendeleza tasnia hii ya fim na kwakweli nawashukuru sana maana wao ndio kwa namna moja au nyengine wamenisaidia sana.

nikiwa na lukas ambae ni mzaliwa wa south africa na ameshiliki katika tamthilia ya isidingo

nikiwa pa Emmanuel Myamba


5.       KUHUSU FAMILIA YANGU.
Kwa upande wa familia kwakweli sina budi kumshukuru Mungu sana kwa ulinziwake waajabu ambao ametutendea na anaoendelea kututenedea kila kukicha. Familia imekua kwa badezote salama sana hasa kwenye upande wa afya, uchumi na huduma. Upande wa baba yangu yeye amekua salama na kuzidi kuihubiri ijili kwa watu ambao bado hawaja fikiwa katika kila pade na bado ataendelea maana ndio kitu akicho itiwa, mamayangu pia ndivyo hivyo hivyo na kubwa zaidi ni mwishoni mwa mwaka amepata shahadayake ya kuhitimu mafunzo ya theologia katika chuo cha Nehemia bible instute chenye makao makuu nchini Kenya. Kaka yangu yeye anaendelea vizuri na mwaka 2011 amefanikiwa kuongeza familia na sasa anamtoto wapili ambae anaitwa Eric kwahio sasa sio watatu bali ni wanne yaani watoto 2 na wazazi 2. Mdogo wangu  ambae pia ni mwanamziki wa kutegemewa hapa kisiwa ni amefanikiwa kujenga studio yake ambapo ina karibia kuisha mda mfupi ujao mana iko katika harakati za kuisha, wasanii wote mnakaribishwa katika studio hii ambayo itakua ni yakwanza kwa uzuri Zanzibar na ina vifaa vya uhakika. Wadogo zangu wawili yaani Neema na Yosia nao wao wanaendelea na kuchimba kitabu na wanafanya vizuri katika matokeo wanashika nafasi ya 1-2. Namimi ndo hivyo namshukuru Mungu naendelea vizuri .
kaka ynagu philemon na familia yake.

mama alipo kua katika maafari yake

mdogo wang lucky boy

studio tarajiwa

6.       WAZO LANGU
Jamani mimi ninaomba kwa wote ambao tupo kwa ajili ya kupambana na umasikini pamoja na tunao tafuta maisha bora kwa familia zetu na kwataifa kwa jumla. Tujiadhari sana na kutopenda maeneleo ya mtu hasa tunapo ona mwenzetu amefanikiwa, mi ndadhani njia nzuri ni kufanya kazi kwa bidii na kama tutamuona mwenzako kafanikiwa kuliko wewe basi nawewe jitahidi kufayakazi ili niweze kumfikia au kumzidi kabisa, ila tusiwe watu wakuvunjishana moyo, kumdharau mwenzio kwa anacho kifanya, kumuona mwenzio hafai na hawezi kua kama wewe, majungu, uchawi, fitina na kila jambo ambalo halifai. Mi nadhani tukiachana na hayo basi tuna weza kua katika hatua nzuri.

Mastaa wa film, bongo flaver, gospel,dansi na kadhalika jamani kumbukeni mlipotoka sio leo tayari umekua na jina ndio uone wengine hawafai.  dharau kwa wasanii wadogo sio kitu kizuri hebu katika mwaka 2012 tushilikiane kwa pamoja na tuwanyanyue wote ambao ni wasanii wenye vipaji na kuwapa msaada hata wakimawazo mana nimetembea na nime ona katika makundi madogo madogo watu wenye vipaji wapo ila hakuana wakuwasukuma na wakuwasukuma sio selikali ila ni sisi wasanii kwa wasanii hata kwa mawazo. Kubwa kuliko yote tusidharau wananchi yaani mashabikiwetu maana wao ndio wanao kufanya wewe uwe hivyo hebu tuweke utaratibu hata wakupata nafasi ya kusikiliza mawazo yao katika sehemu zao husika mana naamini wao wanamengi ya kusha uri.

Nawatakia heri ya mwaka mpya na Mungu wagu wa mbiguni awabariki na kuwalinda, Amen

No comments:

Post a Comment