Katika maisha hakuna kitu kizuri kama kumsaidia mtu ambae hana uwezo wa kufanya kitu Fulani hasa pindi mtu huyo anapo kua na shida sana, pindi utakapo msaidia shukurani yake itakua ya kutoka moyoni na sio yeye tu hata Mungu atakubarikia kupitia huduma hio ulio ifanya mana ndio maana alituweka duniani ili tusaidiane. Na kwa kumaanisha hilo akaweka mwanaume na mwanamke yaani watu wawili ambao waishi kwakusaidiana na sio msaada ule ambao wengi wanaufikilia tu bali ni msaana wowote ambao kama mwenzio hawezi basi mwengine amuwezeshe.
Kila siku ya jumamosi ya mwisho mwezi hua tuna fanya kazi ya kusaidia watoto mayatima na wasio jiweza katika vijiji ambavyo vipo hapa Zanzibar na kawakweli maisha ambayo wana ishi watoto hawa niyakusikitisha na yakuhitaji msaada. Mimi mwenyewe kushilikiana na Mchungaji Philemon na Lameck tumeanza huduma hio kwa kusaidia watoto yatima na wasio jiweza kwa kutoa tulicho nacho na kwanguvuzetu sisi wenye…….. Saidia watoto wa sasa ujenge taifa la baadae ambalo litaishi kwa maendeleo yalio toka katika msaada wako maana kila mtu alipo au alipofikia kwa vyovyote itakua kuna mtu au kitu kilimsaidia mpaka ukafika katika hatua ambayo ukonayosasa. Karibu Zanzibar karibu kusaidia jamii inayo hitaji msaada wako.
Hapa ndio nyumba ya kwanza ambayo tulianza kufikia na mwezi huu tulikua na wageni kutoka global challenge walifika na kuungana nasi katika kuona hali halisi ambayo tuna kutana nayo napia ni jinsi gani ambavyo tuna fanya kazi hii.
Mr lameck akitoa maelekezo kidogo ni namnagani tutaanza na jinsi mpangilio mzima wa shughuli yetu itakavyo kua.
Mara moja tulianza huduma hii na mimi mwenyewe ndio nikawapa watoto hawa wa nyumba hii zawadi ambapo watoto hawa wanaishi na mama pekeyake pamoja na babu yao na familia nzima haina kazi maana baba wa watoto hawa aliwakimbia tokea wakiwa bado wadogo na hajulikana yuko wapi. Kwakweli watoto hawa wanaishi kwa tabu sana.
Hii ni familia nyengine tena ya watoto hawa ambao wanaishi bila wazazi na kama unavyo ona maisha wanayo ishi ni yakusikitisha. The one nikiwa kama kawaida yangu niki wapa zawadi.
Familia hii ina watoto wane ila tulimkuta mmoja tu na wengine walikua wameenda kufanya vibarua kwa ajili ya kupata pesa.
Hapa tulifika katika familia nyengine ila tuka wa tumechoka sana kila mtu aliwa hoi.
Mama huyu analea wajukuu zake nayeye ndio anawasaidia pia na watoto kutokana na ugumu wa maisha inawabini waache shule na kwenda kutafuta vibarua ili kujikimu na maisha ya kila siku.
Mama akituelezea jinsi maisha ya shida anayo ishi katika kijiji hiki na anashukuru kwa kupatiwa msaada.
safari ikiwa inaendelea.
Familia hii ina mtoto mmoja na wazazi wake wote wawili ila wazazi hawana uwezo wa kumsomesha mtoto wao na kazi za wazazi wake ni kwenda kulima katika mashamba ya watu wengine kama vibarua. kama mnavyo ona tukiwa tumezunguka na mimi nikiwa nawatafsiria wageni hali halisi tena kwa uyakinifu zaidi.
Te one nikiwa nasikiliza mama wa mtoto akiwa anaelezea hali halisi kwa umakini kabisa. Mama huyu anapenda mwanae asome na awe na halinzuri kama wengine ila uwezo ndo hakuna pia alishukuru sana kwa msaada ambao sisi tuna toa kwa ajili ya mwanae.
Nikitoa zawadi kwa mtoto kama unavyo muona mwenyewe alivyo
hapa ni sehemu ya kucheza bao ambayo baba wa huyu mtoto hua anapendelea kucheza na marafiki zake na mimi kama kawaida yangu huwa sipitwi nikaingia uwanjani... baba wa mtoto ni alie kaa kulia mwenye ndevu.
Hata kama niko kazini bado niliendelea kuweka sawa mambo mengine kwa kuwasiliana na watu sehemambalimbali. Kama unavuona sim inaniweka bize muda wote.
Eeee hii ni familia nyengine na haya ndio maisha. Halisi ya sehemu hii
Hapa tulifika katika familia nyengine ila tuka wa tumechoka sana kila mtu aliwa hoi.
Wenzangu wakiwa wamechoka.
The one …. Simple man by nature nikiwa nimechoka sana
mama muhusika akisalimia.
Lakini kazi ikaendelea nikawa kama kawaida. Na tulifanya hivyo kwa kila familia.
Eeeee kazi inaendelea.
sehemu nyengine hii jamani kama uonavyo watu tukiendeleza mzigo kwa raha na masikitiko yetu.
vijana tumefika kwa upendo na furaha kuu.
watoto wakipata zawadi kwakweli kwa kila nyumba ambayo hua tunaingia basi inakua furaha na amani na sisi hua tunajisikia raha na furaha tunapokua na watu kama hawa maana tunajua kua hawakupenda ila maisha ndio yamatokea kua hivi..........
ikanilazimu nipige picha na hawa watoto kwa kupata ukumbusho maana kazizao ni kuuza nazi na pia wanavunja kokoto wakimsaidia mama yao ili maisha yasonge mbele. eeeee
hapa ndio nyumabani kwao na huyo ndio mama yao na hio ndio nyumbayao
No comments:
Post a Comment