FROM ZANZIBAR
BY
Emmanuel Obeid Fabian |
Baada ya taarifa mbalimbali za kifo cha Muigizaji mashughuli na kinara wa film Tanzania. Hayati Steven Charles Kanumba “KANUMBA THE GREAT”. Leo ndio tume muaga na kukubaliana na hali halisi maana siku zote ukweli utasimama katika kweli.
Kanumba alie zaliwa mnamo waka 1984 na kufariki mwaka huu wa 2012 yaani ni muda mchache ambao tulikua nae na kutarajia mambo mengi kutoka kwake ila Mwenyezi Mungu ameona nivyema ampumzishe kwa wakati huu maana kila kitu kina sababu yake na sote hatujui kwamba ni nini ambacho kingetokea endapo angeendelea kuwepo, ila Mungu ndo anajua na maisha ya watu wote yako mikononi mwa mungu pekee nay eye ndo anajua lini na wakati gani aweze kuvuna.
Kifo nikitu ambacho kinamtokea mtu kwa aina yeke, maana wengine huwa kifo kina wakuta katika ajali ya magari, tren au ndege na wengine hudondokewa na miti au nazi na kuna wengine pia huanguka kutoka sehemumoja mpakanyengine na wengine huuliwa nawatu. Vifo hivyo vyote ni vifo vya ghafla na watu wengi na hata ma star wengi wa ndani na nje ya Africa wamesha pita huko. Pia kipenzi chetu na kioo cha watanzania Mungu amependa aondoke kwa namna hio ambayo imemtokea.
Kanumba alikua rafikiyanu na pia alikua ni mmoja ya walimu wangu wa sanaa japo hatukua na muda mwingi wa kukaa nae ila tulipo kutana alijikuta akiniambia mambo mengi ambayo yalinifanya niwe na hamu ya kufatilia na kujifunza kiundani tasnia hii ya film.
“Dogo mtu asikudanganye katika kazi hii ukitaka kufanikiwa, kwanza ipene kazi hii na waheshimu wanao kuangalia maana hao ndio watakao kuinua au ndio mabosi wako na usitegemee mafanikio ya kazi hii papo kwa papo” hayo ni maneno ya marehemu Kanumba wakati tukiwa tunaongea nae na mara zote alikua akipenda kuniita dogo. Na ni nakumbuka mara ya mwisho kuongea nae tuliongea nae kwenye simu wakati mimi nikiwa nashoot film akaniambia nikimaliza kushoot nimfuate bongo ilituangalie mambo yako vipi.
Wakati marehemu Steven Kanmba akiwa kushoto na Vicent kigosi (Rey)kulia walipokuja kunitembelea na kula pamoja nami chakula cha mchana Zanzibar.
Kanumba alinitoa katika semu moja na kuingia sehemu nyengine. “wakati tunaanza katika ITV watu walikua wanatucheka na kutuita wauza sura ila sasa hivi vile vicheko vya dharau vimekua pongezi na jina langu la Kanumba linajulikana karibia na wapenzi wote wa film nchini” yalikua ni maongezi yake katika maongezi yetu na alichukia sana mtu anae dharau kazi ya film.
Enzi za uhai wake KANUMBA THE GREAT., MOTO WA VOLCANO.
Kwa niaba ya Kundi zima la Extra genius arts group ambalo linafanya kazi yake hapahapa Zanzibar. Tunasema hatuto kusahau kwa mchango wako uliotoa katika kundi hili na daima utaendelea kua mfano katika kundi hili na kubaki mwalimu.
Kundi la Extra genius arts group linatoa pole kwa familia nzima ya Bwana Charles Kanumba na kuomba muwe wavumilivu kwa haya yaliotokea kwani ni mipango ya Mungu na Mungu ndio alimtoa Kanumba kama zawadi na sasa ameamua kumchukua, hatuna la kufanya zaidi ya kumshukuru Mungu.
KWA MAMA WA STEVEN KANUMBA.
Muda mwingi alikutaja katika mazungumzo yake hasa akiwa anaongelea stori ya maisha yake. Tunajua ni kiasi gani ulivyokua na maumivu ambayo nivigumu kutamka ila mama tuna kupa pole sana maana wewe ndo unamjua kuliko hata sisi sote tumjuavyo. Mungu akupe uvumilivu mkuu na siku moja tutakutana nae katika uzima ule wa milele ambapo kilio na majonzi yahata kuwepo tena.
MUNGU aiweke roho ya Steven Charles Kanumba mahali pema peponi AMEN.
R.I.P STEVEN KANUMBA
No comments:
Post a Comment